Timu ya Zanzibar Heroes imeanza vyema michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rwanda 'Amavubi' mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kenyatta akaunti ya Machakos.
Matokeo hayo yanaifanya Zanzibar kuwa vinara wa kundi A ikiwa na pointi tatu sawa na wenyeji Kenya lakini ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
Zanzibar wanaofundishwa na kocha Hemed Moroco walicheza mechi hiyo kwa kasi na maelewano makubwa huku Amavubi wakionekana kushindwa kuhimili vishindo.
Kiungo aliye kwenye kiwango bora kwa sasa Mudathir Yahaya aliifungia Zanzibar bao la kwanza 34 na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo.
Mabao mengine yalifungwa na
Muhammed Juma dakika ya 52
Kassim Khamis dakika ya 82 wakati bao la kufutia machozi la Amavubi likiwekwa kambani Muhadjire Hakizimana dakika ya 47.
Mchezo unao endelea kwa sasa ni baina ya wenyeji Kenya dhidi ya Libya katika kundi hilo hilo la A.
ZANZIBAR YATOA ONYO CHALENJI, YAFANYA MAUJI YA KUTISHA
Title: ZANZIBAR YATOA ONYO CHALENJI, YAFANYA MAUJI YA KUTISHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Zanzibar Heroes imeanza vyema michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rwa...
Hongera Zanzibar Starz hii kasi iendelee.
ReplyDelete