SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NINJE: ITAKUWA AIBU KUONDOKA CHALENJI NA POINTI MOJA TU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda mchezo wa mwisho dhidi ya wenyeji Kenya katika...
Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda mchezo wa mwisho dhidi ya wenyeji Kenya katika mechi ya kukamilisha ratiba hii leo.

Ninje amesema litakuwa suala la aibu kama wataondoka kwenye michuano ya Chalenji wakiwa na pointi moja hivyo amewataka wachezaji wahakikishe wanafanya kila linalowezekana ili kushinda mchezo wa leo.

Kili Stars inaburuza mkia katika kundi A ikiwa na pointi moja baada ya kupokea vipigo viwili kutoka kwa Zanzibar na Rwanda huku wakiambulia sare kwenye mchezo dhidi ya Libya.

"Nimeongea na wachezaji wangu kuwaambia kuwa wanatakiwa kushinda mchezo wa leo ili kuepuka aibu ya kuondoka na alama moja kwenye michuano hii.

"Nimewataka kujituma kama tunapaswa kusonga mbele ingawa sio hivyo kwakua itakuwa aibu kama tutaaga mashindano tukiwa na pointi moja tu," alisema kocha Ninje.

Kocha Ninje amekuwa akilalamikiwa na Watanzania kutokana na matokeo mabaya ya Kili Stars kwakua walitarajia kuona inafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top