Manchester United imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwq Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford.
Matokeo hayo yanaifanya City kuwa mbele kwa alama 11 dhidi ya United wanaoshika nafasi ya pili huku zikibaki mechi mbili kukamilisha mzunguko wa ligi hiyo.
City kama kawaida walitawala mchezo na kufika zaidi langoni mwa United na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 43 lililofungwa na David Silva.
Katika dakika nne za nyongeza kipindi cha kwanza United walisawazisha bao hilo kupitia kwa Marcos Rashford baada ya kupokea pasi ndefu ya Nemanja Matic.
Mlinzi Nicholas Otamendi aliipatia City bao la pili dakika ya 53 baada mpira wa adhabu uliopigwa na Silva kabla ya kumkuta mfungaji huyo.
City ipo kileleni mwa msimamo na pointi 46 ikifuatiwa na United yenye alama 35.
MAN UNITED YASHINDWA KUIZUIA CITY OT YAPATA KIPIGO
Title: MAN UNITED YASHINDWA KUIZUIA CITY OT YAPATA KIPIGO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Manchester United imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwq Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika kwenye uwan...
Post a Comment