Timu ya Liverpool imetoka sare ya bao moja dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi ya Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa Anfield.
Mchezo huo hujulikana kwa jina la Merseyside Derby kwakua timu hizo kutoka katika mji huo ambapo kwa kawaida huwa mechi huwa ngumu.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mohamed Salah dakika ya 42 baada ya kumalizia pasi ya mlinzi Joel Gomez.
Wayne Rooney alifunga bao la kusawazisha dakika ya 77 kwa mkwaju wa penati na kuzifanya timu hizo kugawana pointi.
Rooney alikuwa akicheza mechi hiyo baada ya miaka 13 kufuatia kujiunga na Manchester United mwaka 2004 ambapo baada ya kurejea amefunga bao la kusawazisha.
Katika mchezo wa awali Southampton imeibana Arsenal kwa kutoka sare ya bao moja katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la St Mary's.
Muda mfupi ujao Manchester United itakuwa Old Trafford kuwakaribisha majirani zao Manchester City katika muendelezo wa ligi hiyo.
LIVERPOOL NAYO YANG'ANG'ANIWA MERSEYSIDE DERBY
Title: LIVERPOOL NAYO YANG'ANG'ANIWA MERSEYSIDE DERBY
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Liverpool imetoka sare ya bao moja dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi ya Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa Anfield. Mch...
Post a Comment