Bondia Tyson Fury anaamini kocha Jose Mourinho ni mshindi kama yeye na ataiongoza Manchester United kuifunga City kwenye uwanja Old Trafford usiku wa leo.
Fury ambaye anasubiri rufaa yake ya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni kusikilizwa kabla ya kurejea tena ulingoni ni shabiki wa United tangu akiwa mtoto na anaamini licha ya City kuwa kwenye ubora mkubwa lakini hawawezi kushinda katika dimba la Old Trafford leo.
"Nitakuwepo uwanjani na rafiki zangu kuangalia kinachotokea, napenda kuangalia mechi za United kila ninapopata nafasi.
"Kuna Derby nyingi nzuri za soka kwa mwaka lakini hii huwa sipendi kuikosa kabisa napenda niwepo uwanjani.
"Mourinho amefanya vizuri akiwa na timu tofauti, ni Meneja mzuri na anafanya vizuri msimu huu na ataendelea kufanya hivyo ingawa anahitaji kupewa muda.
"Kama nilivyo mimi, Mourinho ni mshindi haitaji kuhamasishwa kabla ya mchezo anapenda kuwa juu muda wote na ndio kinachomfanya kufanya vizuri," alisema Fury.
FURY AIPA USHINDI UNITED MBELE YA CITY OLD TRAFFORD LEO
Title: FURY AIPA USHINDI UNITED MBELE YA CITY OLD TRAFFORD LEO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Bondia Tyson Fury anaamini kocha Jose Mourinho ni mshindi kama yeye na ataiongoza Manchester United kuifunga City kwenye uwanja Old Traffo...
Post a Comment