Winga wa timu ya Vipers FC, Milton Kalisa ambaye anaiwakilisha nchi ya Uganda kwenye michuano ya Cecafa Chalenji amekiri kuwa ana ndoto ya kuchezea timu ya Tusker FC ya Kenya tangu akiwa kijana mdogo.
Kalisa ni mmoja wa nyota wanaotegemewa na kocha Moses Basena ambapo amecheza michezo yote ya hatua ya makundi huku pia mchango wake ukihitajika kwa ajili ya kutetea taji hilo waliolitwaa mwaka 2015.
Winga huyo ambaye ameisaidia timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali amesema ikitokea ofa ya Tusker hatofikiria mara mbili badala yake atajiunga moja kwa moja.
"Tumekuja hapa kutetea ubingwa wetu na mpaka sasa mambo yanaenda kama yalivyopangwa na tunaweza kutetea taji hili.
"Hapa Kenya kuna klabu kubwa nyingi lakini nikiambiwa nichague moja nijiunge nayo nikitoka Vipers basi itakuwa Tusker naipenda hii timu," alisema Kalisa
NYOTA WA UGANDA AFUNGUKA KUWA ANAITAKA TIMU HII...
Title: NYOTA WA UGANDA AFUNGUKA KUWA ANAITAKA TIMU HII...
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Winga wa timu ya Vipers FC, Milton Kalisa ambaye anaiwakilisha nchi ya Uganda kwenye michuano ya Cecafa Chalenji amekiri kuwa ana ndoto ya...
Post a Comment