SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KILI STARS SIKIO LA KUFA YAPIGWA TENA CHALENJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars' imepoteza mchezo wa pili katika michuano ya Chalenji na kuopoteza kabisa matumaini ya kusonga ...

Timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars' imepoteza mchezo wa pili katika michuano ya Chalenji na kuopoteza kabisa matumaini ya kusonga mbele kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Rwanda.

Kili Stars imebaki na alama moja na ndio inaburuza mkia kwenye kundi A huku ikibakiwa na mchezo mmoja ambao itacheza na wenyeji Kenya siku ya Jumatatu.

Rwanda walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa na Innocent Nshitu baada ya kumzidi ujanja mlinzi Mohammed Hussein.

Mshambuliaji Danny Lyanga aliisawazishia Kili dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Abdul Hilal kabla ya Abedy Biramihere kufunga bao la ushindi dakika ya 66.

Endapo Kenya itaibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Zanzibar itakuwa imeipa tiketi Kili Stars ya kuaga mashindano hayo rasmi kwani hata akishinda mechi ya mwisho bado hawezi kufika popote.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top