SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AJIBU: TUNAENDA KUJIPANGA KWA MASHINDANO YAJAO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Ibrahim Ajibu amesema baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Chalenji wanarudi nyumbani ...
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Ibrahim Ajibu amesema baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Chalenji wanarudi nyumbani kujipanga na mashindano yajayo.

Kesho Kili Stars itacheza mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya wenyeji Kenya ambapo hata kama watashinda hawawezi kufuzu katika hatua ya nusu fainali.

Ajibu ambaye katika mchezo wa jana waliopoteza kwa mabao 2-1 kutoka kwa Rwanda alichaguliwa mchezaji bora wa mechi alisema haikuwa bahati ila kwa sasa wanajipanga kwa mashindano mengine.

"Tumeshindwa kusonga mbele lakini sio mwisho wa soka, tunarudi nyumbani kujipanga kwa mambo mengine," alisema Ajibu.

Kabla ya kuanza michuano hiyo Disemba tatu mwaka huu Kili Stars ilikuwa moja ya timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo lakini haijashinda hata mchezo mmoja mpaka sasa.

Kili Stars inaburuza mkia ikiwa na alama moja wakati majirani zao Zanzibar Heroes wametinga nusu fainali ikiwa kinara wa kundi A na pointi saba.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top