Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametangaza kuwasamehe familia ya mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanaye Papii Kocha ambao walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha gerezani.
Rais wa Magufuli alitoa msamaha huo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika mjini Dodoma leo.
Rais Magufuli pia ametangaza kusamehe wafungwa 8,157, na kuagiza wafungwa 1,828 kati yao watolewe magerezani mara moja na waliobaki wapunguziwe muda wa kukaa gerezani ili waje watolewe kwa mujibu wa vifungo vyao.
Rais pia ametangaza kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa, na kuagiza watolewe gerezani leo au kesho.
RAIS MAGUFULI AMUACHIA HURU BABU SEYA NA FAMILIA YAKE
Title: RAIS MAGUFULI AMUACHIA HURU BABU SEYA NA FAMILIA YAKE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametangaza kuwasamehe familia ya mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya...
Post a Comment