Kiungo mshambuliaji Phillipe Coutinho amefunga mabao matatu 'hat tick' wakati timu yake ya Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Spartak Moscow katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Anfield ambapo vijana wa kocha Jurgen Kloop wakicheza soka safi huku ikionekana ni mechi ya upande mmoja.
Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Sadio Mane aliyefunga mawili wakati Roberto Firmino na Mohamed Salah wakifunga moja kila mmoja.
FC Porto nayo imetoa dozi nene baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Monaco wakati mabingwa watetezi Real Madrid ikishinda mabao 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund.
Manchester City imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka Shakhtar Donetsk wakati Tottenham Hotspur imeifunga APOEL Nicosia mabao 3-0
Matokeo kamili ya michezo yote ya UCL
Liverpool 7-0 Spartak Moscow
Maribor 1-1 Sevilla
Feyenoord 2-1 SSC Napoli
Shakhtar Donetsk 2-1 Man City
FC Porto 5-2 Monaco
RB Leipzig 1-2 Besiktas
Real Madrid 3-2 Borussia Dortmund
Tottenham Hotspur 3-0 APOEL Nicosia
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Anaefatia anakula wiki tena..ynwa
ReplyDelete