Kocha mkuu wa timu ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' Ammy Ninje amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo dhidi ya Zanzibar na maandalizi yamekamilika kuhakikisha wanashinda.
Mchezo huo wa kundi A utafanyika kwenye uwanja wa Kenyatta mjini Machakos wakati mashabiki kutoka bara na visiwani wakiusubiri kwa hamu kubwa kutokana na uwezo mkubwa ulioonyeshwa na vijana wa kocha Hemed Morocco.
Zanzibar ina pointi tatu ikishika nafasi ya pili kwenye kundi hilo baada ya kuifunga timu ya Rwanda 'Amavubi' mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza wakati Kili Stars ilitoka sare ya bila kufungana na Libya.
Kocha Ninje amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo katika hali nzuri na morali ipo juu kuhakikisha wanapata pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuvuka hatua hiyo.
"Mchezo utakuwa mgumu Zanzibar wana kikosi kizuri na wanacheza kitimu ila tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda katika hali yoyote," alisema Ninje.
Endapo mchezo huo utamalizika kwa sare au Kili Stars kupoteza itakuwa imejiweka kwenye wakati mgumu wa kuvuka hatua ya makundi kwani itakuwa imebakiwa na mechi mbili dhidi ya wenyeji Kenya na Rwanda.
NINJE: ZANZIBAR NJOONI TUKO TAYARI
Title: NINJE: ZANZIBAR NJOONI TUKO TAYARI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa timu ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Stars' Ammy Ninje amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo dhidi ya Zanzibar n...
Post a Comment