SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: EXCLUSIVE ATUPELE ATUA KAGERA SUGAR
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji Atupele Green amejiunga na Kagera Sugar kwa mkataba wa miezi sita siku chache baada ya kuachana na Singida United. Nyota hu...
Mshambuliaji Atupele Green amejiunga na Kagera Sugar kwa mkataba wa miezi sita siku chache baada ya kuachana na Singida United.

Nyota huyo wa zamani wa timu za Ndanda FC na Ruvu Shooting ametumia miezi sita tu katika mkataba wake wa miaka miwili lakini baada ya kukosa uhakika kwenye kikosi cha kwanza ameamua kutimka.

Tangu kuondoka kwa mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyejiunga na Azam FC, Kagera imekuwa ikipata shida ya kufunga huku ikianza msimu kwa kusuasua hivyo wameona Atupele anaweza kuziba pengo lake.

Kiongozi mmoja wa timu hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake kwenye mtandao huu amesema kuwa nyota huyo amesaini mkataba wa miezi sita utakao muweka hadi mwishoni mwa msimu.

"Atupele amejiunga nasi na tutakuwa nae mpaka mwishoni mwa msimu na taarifa rasmi itatolewa muda wowote kutoka sasa," alisema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo amesema ndani ya siku chache zijazo watasajili wachezaji wawili kutoka timu za Simba na Yanga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top