Meneja wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amembadili namba Mathieu Debuchy katika aina yake ya kuchezesha mabeki watatu wa kati, ikijiandaa na mchezo dhidi ya Manchester City Jumapili ijayo.
Tangu raia huyo wa Ufaransa alipojiunga na Arsenal mwaka 2014, ameshinda kupata namba ya moja kwa moja kutokana na kuandamwa na majeruhi ya nyama za paja ambapo msimu uliopita alicheza mechi moja pekee.
Debuchy amekuwa akipata nafasi kwenye michezo ya Europa na kombe la ligi 'Carabao Cup' ambapo Wenger anaona akitumia mabeki watatu wa kati, beki huyo wa kulia atakuwa na nafasi ya kudumu akiwa beki wa kati.
Wenger alisema "Nadhani atakuja kuwa beki mzuri wa kati. Anafanya kazi kubwa licha ya kuwa na mwili mdogo ila ni mzuri pia hewani.
"Unaweza ukafikiria hawezi kuwa beki wa kati sababu ni mfupi, lakini ukihesabu mipira anayoishinda hewani utaona ni jinsi gani alivyo katika ubora."
Wenger amemwagia sifa beki huyo ambaye katika usajili wa mwezi Januari mwaka huu alimwambia yuko huru kutimka kwa Washika bunduki hao
WENGER AMFANYA DEBUCHY KUWA BEKI WA KATI
Title: WENGER AMFANYA DEBUCHY KUWA BEKI WA KATI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amembadili namba Mathieu Debuchy katika aina yake ya kuchezesha mabeki watatu wa kati, ikijiandaa...
Huyu babu akili zake anazijua mwenyewe sasa kwa nini alimuuza Gabriel fwala sana huyu
ReplyDelete