SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: UNITED, PSG ZAFUZU 16 BORA ULAYA, CHELSEA YAPATA KIPIGO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu za Manchester United na Paris Saint Germain zimefuzu hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi ul...
Timu za Manchester United na Paris Saint Germain zimefuzu hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi uliowafanya kuongoza makundi yao.

United ndio vinara wa kundi A wakiwa na pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne ikiwemo ya leo ya marudio waliobuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Benifica ya Ureno mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford.

Katika mchezo huo mabao ya United yalifungwa na mlinda mlango Mile Svilar aliyejifunga na mlinzi Daley Blind kwa mkwaju wa penati.
PSG nao wana pointi 12 kama United wakiongoza kundi B kufuatia ushindi wa mabao 5-0 walioifunga timu ya Anderlecht ya Ubelgiji mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Parc des Princes.
Chelsea imekubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa AS Roma ya Italia katika mchezo wa kundi C ambapo vijana hao wa kocha Antonio Conte walizidiwa sehemu kubwa na kushindwa kufurukuta.

Matokeo kamili ya michezo iliyopigwa

Basel 1-2 CSKA Moscow

Man United 2-0 Benfica

Celtic 1-2 Bayern Munich

PSG 5-0 Anderletch

Atletico Madrid 1-1 Qarabag FK

Roma 3-0 Chelsea

Olympiacos 0-0 Barcelona

Sporting CP 1-1 Juventus

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Mara Paaap Manchester vs Madrid/Barcela hatua inayofuata maana naona hawa wahispania wanajilegeza makusudi kumsaka chamdomo wamzibue teeeeh

    ReplyDelete

 
Top