Nyota wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid utakaofanyika kesho kwenye uwanja wa Wembley.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza alikosa mchezo wa Jumamosi iliyopita waliopoteza kwa bao moja dhidi Manchester United kufuatia maumivu ya nyama za paja aliyopata katika mechi waliyoshinda mabao 4-1 mbele ya Liverpool.
Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amesema kuwa ana matumaini ya kumtumia nyota huyo mwenye miaka 24 katika mechi dhidi ya miamba hiyo Hispania.
"Nadhani madaktari na mchezaji mwenyewe watafanya maamuzi sahihi, tutamuangalia kwanza hali yake kabla ya kufanya maamuzi.
"Najisikia vizuri lakini sio maneno yangu ni Harry Kane, yuko vizuri," alisema Pochettino.p
Spurs ni vinara wa kundi H wakiwa na pointi saba sawa na Madrid wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga ikishinda mechi mbili na kutoka sare moja.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
KANE AREJEA, KUIKABILI REAL MADRID KESHO
Title: KANE AREJEA, KUIKABILI REAL MADRID KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyota wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid utakaofanyika...
Post a Comment