Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa
klabu ya Simba, Hajji Manara amelalamika kuwa waamuzi wamekuwa wakiwahujumu
katika mchezo yao ya ligi.
Manara amesema kuwa wameandika barua kwa bodi
ya ligi (TPLB) kuhusu malalamiko yao ambapo katika michezo dhidi ya Mbao
walinyimwa penati mbili, Stand United ilipewa penati isiyo halali na katika
mechi ya Yanga pia walinyimwa penati mbili.
Manara amewaonyesha picha za video Waandishi
wa habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika michezo yao mitatu
iliyopita na kuwataka waamuzi kuchezesha kwa kufuatia sheria 17 za soka.
"Tumeandika barua kwa bodi ya ligi kutoa
malalamiko yetu kuhusu hujuma dhidi yetu, waamuzi wamekuwa wakitunyima penati
tunataka mpira uchezeshwe kwa haki," alisema Manara.
Msemaji huyo alisema anajua kauli hiyo inaweza
kumuweka matatani na pia kumfanya kufungiwa lakini hilo halimtishi na anatetea
kibarua chake.
Post a Comment