SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA KUWAIBUKIA MBEYA CITY IJUMAA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka Ijumaa kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mbeya City utakaofanyika kwenye uwanja...
Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka Ijumaa kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mbeya City utakaofanyika kwenye uwanja wa Sokoine siku ya Jumapili.

Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo nane. Vijana hao wa kocha Joseph Omog wameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo jana ambapo ukiacha wachezaji Shomari Kapombe, Salim Mbonde na mlinda mlango Said Mohammed 'Nduda' hakuna mwingine ambaye ni majeruhi.

Msemaji wa klabu hiyo, Hajji Manara amesema kuwa kikosi chao kinaendelea kujifua hapa jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo siku tatu zijazo.

"Kikosi kimeanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo dhidi ya City na kitaondoka siku ya Ijumaa tayari kwa mechi ya Jumapili.

"Nimeongea daktari mpaka sasa hakuna mchezaji mwingine ambaye ni majeruhi ukiacha wakina Kapombe, Mbonde na Nduda," alisema Manara.


Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao moja na watani wao Yanga wikiendi iliyopita

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Ijumaa.afu jpili mechi.....je watarnda.kwa usafiri gani....kama.ni bus watachoka..

    ReplyDelete

 
Top