Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka Ijumaa
kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mbeya City
utakaofanyika kwenye uwanja wa Sokoine siku ya Jumapili.
Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na
pointi 16 baada ya kucheza michezo nane. Vijana hao wa kocha Joseph Omog wameanza
mazoezi kwa ajili ya mchezo huo jana ambapo ukiacha wachezaji Shomari Kapombe,
Salim Mbonde na mlinda mlango Said Mohammed 'Nduda' hakuna mwingine ambaye ni
majeruhi.
Msemaji wa klabu hiyo, Hajji Manara amesema
kuwa kikosi chao kinaendelea kujifua hapa jijini Dar es Salaam kabla ya
kusafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo siku tatu zijazo.
"Kikosi kimeanza mazoezi jana kujiandaa
na mchezo dhidi ya City na kitaondoka siku ya Ijumaa tayari kwa mechi ya
Jumapili.
"Nimeongea daktari mpaka sasa hakuna
mchezaji mwingine ambaye ni majeruhi ukiacha wakina Kapombe, Mbonde na
Nduda," alisema Manara.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na
kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao moja na watani wao Yanga wikiendi
iliyopita
Ijumaa.afu jpili mechi.....je watarnda.kwa usafiri gani....kama.ni bus watachoka..
ReplyDeletewanaondoka na ndege
Delete