Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya, Real Madrid itakuwa ugenini kutetea taji lake kwa kucheza na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Kundi H utakaofanyika kwenye uwanja wa Wembley usiku wa leo.
Madrid wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbumbuku ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Girona ambayo imepandanda daraja msimu huu walichokipata wikiendi iliyopita.
Vijana hao wa kocha Zinedine Zidane 'Zizzou' wamesafiri mpaka jijini London bila nyota wao Gareth Bale na mlinda mlango Kaylor Navas ambao ni majeruhi. Kwa upande wa Spurs wao wanafurahi urejeo wa nyota Harry Kane aliyekuwa majeruhi na kiungo Dele Alli aliyemaliza kutumikia adhabu yake.
Timu hizo zilizo kundi H zina pointi saba kila moja zikiwa sawa pia katika idadi ya mabao ya kufunga. Spurs nayo inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao moja kutoka kwa Manchester United ilichokipata Jumamosi iliyopita.
Manchester City ambayo ipo kwenye kiwango bora kwa sasa nayo itakuwa ugenini kucheza na SSC Napoli ya Italia ambapo katika mchezo uliopita ilishinda mabao 2-1.
Liverpool itakuwa Anfield kuwakaribisha Maribor ya Slovenia ambayo katika mchezo uliopita ilishinda mabao 7-0.
Ratiba ya mechi zote za ligi ya mabingwa zitakazofanyika usiku wa leo
Liverpool vs Maribor
Sevilla vs Spartak Moscow
SSC Napoli vs Manchester City
Shakhtar Donetsk vs Feyenoord
Besiktas vs Monaco
FC Porto vs RasenBallsport Leipzig
Borussia Dortmund vs APOEL
Tottenham Hotspur vs Real Madrid
MADRID KULIPA KISASI CHA GIRONA, KWA SPURS LEO?
Title: MADRID KULIPA KISASI CHA GIRONA, KWA SPURS LEO?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya, Real Madrid itakuwa ugenini kutetea taji lake kwa kucheza na Tottenham Hotspur katika...
Post a Comment