Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samata anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ametajwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowania tuzo za mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017.
Samata ambaye amekuwa ni moja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Genk atapambana na nyota wenye majina makubwa wanaocheza barani Ulaya kama Mohammed Salah, Pierre-Emerick Aubameyang, Sadio Mane, Erick Bailly n.k
Mtanzania huyo alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2016 kwa wachezaji wa ndani wakati akiichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo.
Michael Olunga kutoka Kenya ambaye anachezea Girona ya Hispania nae ametajwa katika orodha hiyo hivyo ukanda wa Afrika Mashariki una wawakilishi wawili.
Kura zitapigwa na makocha na wakurugenzi wa timu za taifa, wajumbe wa kamati za ufundi za CAF pamoja na Waandishi wa habari.
Orodha kamili ya wachezaji wanaowania tuzo hizo ni pamoja na
1. Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)
2. Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon)
3. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)
4. Christian Atsu (Ghana & Newcastle)
5. Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye)
6. Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United)
8. Essam El Hadary (Egypt & Al Taawoun)
9. Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla)
10. Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco)
11. Jean Michel Seri (Cote d’Ivoire & Nice)
12. Junior Kabananga (DR Congo & Astana)
13. Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord)
14. Keita Balde (Senegal & Monaco)
15. Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor)
16. Mbwana Samata (Tanzania & Genk)
17. Michael Olunga (Kenya & Girona)
18. Mohamed Salah (Egypt & Liverpool)
19. Moussa Marega (Mali & Porto)
20. Naby Keita (Guinea & RB Leipzig)
21. Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns)
22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
23. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
24. Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid)
25. Victor Moses (Nigeria & Chelsea)
26. Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto)
27. William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor)
28. Yacine Brahimi (Algeria & Porto)
29. Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail)
30. Yves Bissouma (Mali & Lille)
Tuzo hizo zitatolewa Alhamisi ya Januari, 4 mwakani katika jiji la Accra nchini Ghana.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment