SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MADRID YACHANIA WATU MIKEKA YAO YAPATA KIPIGO TOKA SPURS
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Real Madrid imekubali kipigo cha pili ndani ya siku tatu kufuatia kufungwa mabao 3-1 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa ligi ya mabingw...
Real Madrid imekubali kipigo cha pili ndani ya siku tatu kufuatia kufungwa mabao 3-1 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.

Jumapili iliyopita Real walikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Girona katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania.

Matokeo hayo yanaifanya Spurs kuwa vinara wa kundi H wakiwa na pointi 10 baada ya mchezo minne na kuizidi miamba hiyo ya Hispania alama tatu.

Kiungo Dele Alli ambaye ametoka kifungoni alifunga mabao mawili na Eriksen huku Cristiano Ronaldo akifunga la kufuatia machozi la Madrid.
Liverpool nayo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Maribor wakati Manchester City imeifunga Napoli mabao 4-2.

Shakhtar Donetsk imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Feyernood ya Uholanzi.

Matokeo kamili ya michezo ya ligi ya mabingwa iliyochezwa leo
Borussia Dortmund 1-1 APOEL

Tottenham Hotspur 3-1 Real Madrid

Liverpool 3-0 Maribor

Sevilla 2-1 Spartak Moscow

SSC Napoli 2-4 Manchester City

Shakhtar Donetsk 3-1 Feyenoord

Besiktas 1-1 Monaco

FC Porto 3-1 RasenBallsport Leipzig


About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. WALICHOKIFANYA SPURS KWA MADRID SI KITU CHA KUKIACHA KIPITE HIVIHIVI.

    SPURS WANASTAHILI ZAIDI YA PONGEZI MAANA KWA HIVI KARIBUNI SIDHANI KAMA KUNA TIMU YA UINGEREZA ILIYOWEZA KUIFUNGA MADRID.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Liverpool ndio ilikuwa timu ya mwisho kuifunga Madrid kwenye michuano ya ulaya,bao 4 za Torres,Gerard na dosena 2

      Delete

 
Top