Meneja wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amesisitiza kuwa timu yake inapaswa kuwekwa miongoni mwa klabu bora barani Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliofanyika jana kwenye uwanja Wembley.
Mabao mawili ya Dele Alli na Christian Eriksen yameifanya Tottenham kuwa vinara wa kundi H wakiwa na pointi 10 na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Vijana hao wa Pochettino wametoka katika vipigo viwili mfululizo kutoka kwa West Ham na Manchester United, lakini kocha huyo raia wa Argentina amesema ushindi dhidi ya Real umewafanya kuwa moja ya klabu bora Ulaya.
"Wote mmeona kuwa Tottenham ni timu kubwa, tumecheza mbele ya mashabiki 80,000 tukaifunga klabu kubwa duniani.Tumeonyesha kuwa Spurs inastahili kuwa bora sio Uingereza pekee bali barani Ulaya.
"Kikubwa ninacho kitazama kwa sasa ni kufuzu hatua ya 16 bora, tulikuwa kwenye kundi gumu ila tumepambana hadi kufika hatua hii," alisema Pochettino.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wana kocha mzuri,wana timu nzuri wakikomaa watafika mbali
ReplyDelete