SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: RATIBA YA LIGI YA VODACOM KUPANGULIWA TENA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara itapunguliwa kupisha michuano ya CECAFA, Chelenji itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba ...
Ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara itapunguliwa kupisha michuano ya CECAFA, Chelenji itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 9.

Michuano ya Chalenji hushirikisha nchi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambayo katika miaka miaka miwili mfululizo hayajafanyika kutokana na kukosa mwenyeji. Katika michuano hiyo Tanzania huwakilishwa na timu za Kilimanjaro heroes kwa bara na Zanzibar heroes kwa Zanzibar.

Kaimu Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema wamethibitisha kushiriki na watapeleka kikosi cha kwanza katika michuano hiyo.

"Tumekuwa tukishiriki michuano ya Chalenji kila mwaka baada ya kukosekana kwa muda kadhaa, CECAFA imetuandika barua na tume thibitisha kushiriki hivyo kwa namna yoyote itaathiri ratiba ya ligi kuu ya Vodacom," alisema Kidao.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema mashindano hayo yalikuwa hayana uhakika wa kufanyika ndio maana hawaku yajumuisha kwenye kalenda yao.

Wambura amesema watawasiliana na klabu kuwajulisha mabadiliko hayo ambapo italazimika ligi kuchezwa hata katikati ya juma ili ratiba isibadilike sana.

"Ratiba ya ligi itabadilika kidogo na hii inatokana na hakukuwa na uhakika wa mashindano haya kama yatakuwepo au la," alisema Wambura.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Africa itabaki kuwa Africa tu,sasa kama hawakuwa na uhakika kwanini waibuke tu ghafla,kwanini wasiipeleke kwenye ratiba ya mwakani tu

    ReplyDelete

 
Top