SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: TANZANIA MWENYEJI MICHUANO YA U17, CECAFA 2018
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Tanzania imepangiwa kuandaa michuano ya vijana ya chini ya miaka 17 katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ijulikanayo kama 'CECAFA...
Tanzania imepangiwa kuandaa michuano ya vijana ya chini ya miaka 17 katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ijulikanayo kama 'CECAFA CAF' itakayofanyika kuanzia mwezi Agosti mwakani.

Michuano hiyo itashirikisha timu nane kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika kwa vijana mwaka 2019 itakayofanyika nchini.

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF limegawa timu zitakazo shiriki michuano hiyo katika kanda ambapo mshindi mmoja wa kila kanda atafuzu moja kwa moja michuano hiyo.

Kaimu katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema Tanzania itashiriki michuano hiyo lakini hata kama itaibuka bingwa atapita mshindi wa pili kwakua imefuzu moja kwa moja kwakua ni timu mwenyeji.

"CAF imetupa uwenyeji wa michuano ya vijana ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati utakaoshirikisha timu nane na moja itafuzu katika michuano ya Afrika itakayofanyika hapa nchini mwaka 2019.

"Mwaka huu CAF imegawa michuano hii katika kanda inaama CECAFA itatoa timu moja COSAFA nayo pia moja na kanda zote Afrika zitatoa timu moja moja ili kufikisha nane," alisema Kidao.

Aidha Katibu huyo amesema watatumia michuano hiyo kuandaa timu yao kuelekea michuano hiyo ambayo watakuwa wenyeji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top