SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: ERASTO MCHEZAJI BORA SIMBA, OKTOBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji aliye kwenye kiwango bora kwa sasa wa timu ya Simba Erasto Nyoni amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Wekundu hao. ...
Mchezaji aliye kwenye kiwango bora kwa sasa wa timu ya Simba Erasto Nyoni amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Wekundu hao.

Simba imekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji bora ambapo safari hii tuzo hiyo imekwenda kwa Erasto ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC atapewa kitita cha sh 500,000 kama zawadi baada ya kushinda tuzo hiyo.

Nyoni amekuwa akihusika moja kwa moja katika ushindi wanaopata timu ya Simba msimu huu huku akiwa ndiye mlinzi anayeongoza kwa kusaidia kupatikana kwa mabao 'Assist' ndani ya klabu hiyo.

Simba imebuni tuzo hizo ili kuhamasisha wachezaji wake kujituma uwanjani ili kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top