Pamoja na
Maafande wa Ruvu Shooting kuwa mkiani katika msimamo wa ligi kuu timu ya Azam
FC itaingia kwa tahadhari kubwa katika mchezo dhidi yao utakaofanyika siku ya
Jumamosi.
Timu hizo
zitakutana katika uwanja wa Azam Complex katika mchezo ambao Ruvu wataingia kwa
nguvu kusaka alama tatu ili kujinasua mkiani.
Ofisa habari
wa Azam FC, Jaffer Idd amesema kucheza na timu inayohitaji pointi kujinasua
mkiani ni ngumu kwa sababu wanatumia nguvu kubwa ingawa wao wamejipanga
kukabiliana nao kwa kila hali.
"Tunawaheshim
Ruvu, wapo mkiani lakini hilo halitupi kujiamini kuwa tutawafunga, tumejiandaa
vizuri kuhakikisha tunatoka na pointi zote kwenye uwanja wetu wa nyumbani ligi
ni ngumu sana msimu huu," alisema Jaffer.
Jaffer
amesema pia walikuwa na mchezo wa kirafiki jana usiku dhidi ya Ashanti United
ili kukiweka sawa kikosi chao kabla ya kuwakabili Ruvu mwishoni mwa juma.
"Tulicheza
na Ashanti jana tukawafunga mabao 4-0. Mabao yalifungwa Idd Kipagwile, Enock
Atta Agyei, Waziri Junior na David Mwantika," alimalizia Jaffer.
Azam ipo
nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 wakati Ruvu ina alama zake tano mkiani.
Post a Comment