Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amesema hakuna mchezaji wa timu hiyo mwenye uhakika wa kujumuishwa kwenye kikosi kitakacho shiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi mwakani.
Southgate, 47, amewajumuisha wachezaji watatu ambao hawakuwahi kuitwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Brazil baadae mwezi huu.
Kocha huyo amesema ataanza kutumia mfumo wa mpya katika michuano hiyo kwa kupanga mabeki watatu wa kati lakini amesisitiza kuwa hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kuwemo katika kikosi chake mwakani.
"Kama nikiambiwa nitaje kikosi kesho nitashindwa kujua nani anafaa kuwemo lakini baada ya miezi sita nitakuwa nimewajua.
Akijibu swali kuwa wachezaji 23 aliowaita kikosini ndio wenye nafasi ya kwenda nchini Urusi, Southgate amesema "Sidhani, kuna wachezaji wengi na kila nafasi uwanjani ina ushindani mkubwa.
"Kasi ya maendeleo ya wachezaji wetu vijana inatia hamasa, hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kuwepo kwenye kikosi kitakacho safiri kwenda Urusi. Majira ya joto yajayo kila kitu kitakuwa hadharani," alisema Southgate.
Mshambuliaji wa Swansea Tammy Abraham, beki wa Liverpool Joe Gomez na kiungo wa Crystal Palace Ruben Loftus-Cheek wameitwa kwa mara ya kwanza wakati winga wa Manchester United, Ashley Young amejumuisha tena kikosini humo tangu mwaka 2013.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
INA MAANA ATA HARY KANE HANA UHAKIKA WA KWENDA URUSI?
ReplyDelete