SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MNYAMA KUPAA MCHANA WA LEO KUWAFUATA MBEYA CITY
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka Dar es Salaam mchana wa leo kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utak...
Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka Dar es Salaam mchana wa leo kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaofanyika kwenye uwanja wa Sokoine keshokutwa Jumapili.

Simba ambayo ndio vinara wa ligi hiyo wana pointi 16 sawa na timu za Mtibwa Sugar, Yanga na Azam lakini ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.

Mchezaji mmoja wa Wekundu hao ambaye hakutaka kutajwa jina kwenye mtandao huu amesema kwa sasa wanaelekea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kabla ya kuondoka saa sita mchana kuelekea jijini humo.

"Hivi tunavyo zungumza tupo njiani kuelekea Airport, ndege itaondoka saa sita kuelekea Mbeya," alisema nyota huyo.

Msemaji wa Wekundu hao Hajji Manara alinukuliwa na kituo kimoja cha radio asubuhi ya leo na kusema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na maandalizi ya timu zote ingawa wamejipanga kutoka na pointi zote tatu.

"Mchezo utakuwa mgumu, City ni timu nzuri tunaiheshimu lakini nasi tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mchezo huo," alisema Manara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top