Nahodha msaidizi wa timu ya Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Junior' amesema ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji walioupata jana umewaongezea kujiamini kuelekea mechi yao ya watani wa jadi wikiendi ijayo.
Jumamosi Oktoba 28, miamba hiyo ya soka nchini itakutana katika uwanja wa Uhuru mchezo wa kwanza katika mzunguko huu mtanange ambao huwa na presha kuanzia kwa viongozi, wachezaji mpaka mashabiki.
Zimbe amesema maandalizi waliyofanya ndio sababu iliyowafanya kupata ushindi huo ambao utawaongezea morali na hali ya kujiamini kwenye mchezo wa mahasimu wao Yanga.
"Unaposhinda mechi kabla ya mchezo wa watani unaingia uwanjani ukiwa na hali ya kujiamini, mashabiki waendelee kutupa ushirikiano tuna imani tutafanya vizuri pia kwenye mchezo huo," alisema Nahodha huyo.
Simba imeshinda mechi tatu mfululizo dhidi ya watani wao Yanga ukiwemo ule wa mzunguko wa pili msimu uliopita, nusu fainali ya michuano ya mapinduzi na ngao ya jamii iliyofanyika Agosti 23 mwaka huu.
ZIMBWE JR: USHINDI WA JANA UMETUONGEZEA MZUKA
Title: ZIMBWE JR: USHINDI WA JANA UMETUONGEZEA MZUKA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha msaidizi wa timu ya Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Junior' amesema ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji walioupata jan...
Post a Comment