Manchester United imeonja uchungu wa ligi baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Huddersfield Town huku majirani zao Man City wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Burnley.
United haikuwa imepoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo mwezi Agosti ikiwa imetoka sare mara mbili na kushinda mechi sita kabla ya kupokea kipigo hicho jioni ya leo.
Vijana hao wa kocha Jose Mouringo wameonekana kasi yao kuanza kushuka tofauti na walivyoanza huku mshambuliaji wake Romelu Lukaku akishindwa kufunga kwa mchezo wa pili mfululizo.
City imeendelea kujikita kileleni ikiwa na pointi 25 alama tano mbele ya United huku ikiwa pia na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
Mabao ya City yalifungwa na mshambuliaji Sergio Aguero, Leroy Sane na beki Nicholas Otamendi.
Matokeo ya michezo ya ligi ya Uingereza iliyopigwa leo
Chelsea 4-2 Watford
Huddersfield 2-1 Manchester United
Manchester City 3-0 Burnley
Newcastle 1-0 Crystal Palace
Stoke City 1-2 Bournemouth
Swansea City 1-2 Leicester City
UNITED YACHAPWA, CHELSEA, CITY ZAUA EPL
Title: UNITED YACHAPWA, CHELSEA, CITY ZAUA EPL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Manchester United imeonja uchungu wa ligi baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Huddersfield Town huku majirani zao Man City wa...
Post a Comment