Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka jijini Dar es Salaam Jumatatu mchana kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiwinda na mchezo wa watani wao wa jadi Yanga utakaopigwa Oktoba 28 kwenye uwanja wa Uhuru.
Simba imekuwa na desturi ya kuweka kambi visiwani humo kila inapokaribia kucheza na Yanga ambao mara kadhaa nao wamekuwa wakienda Pemba.
Msemaji wa Wekundu hao, Hajji Manara amesema kikosi kamili pamoja na benchi lake la ufundi kitaondoka kwa usafiri wa ndege kuelekea visiwani humo na kitarejea jijini Jumamosi ijayo na kitaenda moja kwa moja katika hotel ya Golden Tulip.
"Kikosi kinaondoka Jumatatu kwa usafiri wa ndege kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Yanga wikiendi ijayo, kikirudi kitakaa kwa muda Golden Tulip kabla ya kwenda uwanjani," alisema Manara.
Manara amesema hatazungumza na chombo chochote cha habari kuanzia leo mpaka mchezo huo wa watani utakapo malizika.
SIMBA KUIENDEA ZENJI YANGA, JUMATATU
Title: SIMBA KUIENDEA ZENJI YANGA, JUMATATU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha timu ya Simba kitaondoka jijini Dar es Salaam Jumatatu mchana kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiwinda...
Post a Comment