SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA YAJIBU MAPIGO YA SIMBA, SASA TUKUTANE OKTOBA 28
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga imejibu mapigo ya watani wao wa jadi Simba baada ya kutoa kipigo cha mabao 4-0 kwa Stand United katika mchezo wa ligi uliofa...
Timu ya Yanga imejibu mapigo ya watani wao wa jadi Simba baada ya kutoa kipigo cha mabao 4-0 kwa Stand United katika mchezo wa ligi uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Jana Simba ilitoa kipogo kama hicho kwa timu ya Njombe Mji kitu ambacho kitaongeza radha kwenye mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa uwanja wa Uhuru wikiendi ijayo.

Huo ndio ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga tangu kuanza kwa msimu huu ambapo wamefikisha pointi 15 sawa Simba wakizidiwa idadi ya mabao ya kufunga.

Mshambuliaji Ibrahim Ajib alifunga mabao mawili katika ushindi huo huku mengine yalifungwa na Pius Buswita na Obrey Chirwa.

Kocha George Lwandamina alifanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake akiwaanzisha mabeki nahodha Nadir Haroub, Hassan Kessi na kiungo Pato Ngonyani ambao walikuwa hawapewi nafasi lakini walionyesha uwezo mkubwa.

Wenyeji walizidiwa sehemu kubwa ya mchezo huo ambapo wanasalia na pointi zao nne wakiwa nafasi ya 15.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top