SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YAMETIMIA! KOEMAN ATUPIWA VIRAGO EVERTON
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Hatimaye klabu ya Everton imemtimua kocha wake Ronald Koeman baada ya kipigo cha mabao 5-2 nyumbani dhidi ya Arsenal nakujikuta wapo kweny...
Hatimaye klabu ya Everton imemtimua kocha wake Ronald Koeman baada ya kipigo cha mabao 5-2 nyumbani dhidi ya Arsenal nakujikuta wapo kwenye nafasi tatu za chini kwenye msimamo.

Klabu hiyo imetangaza maamuzi hayo mchana wa leo baada ya Mwenyekiti wake Bill Kenwright na Mkurugenzi mtendaji Robert Elstone kuwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa mazoezi wa timu hiyo.

Kocha wa timu ya vijana ya miaka 23 David Unsworth atakaimu nafasi hiyo kwa muda ambapo watasafiri kucheza na Chelsea katika kombe la ligi keshokutwa Jumatano kabla ya kukutan na Leicester City Jumapili ijayo.

Everton imefanya usajili wa wachezaji Michael Keane, Davy Klaassen, Jordan Pickford, Gylfi Sigurdsson na Wayne Rooney majira ya joto lakini sasa wapo nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi.

Kipigo cha jana ni cha tano mfufulizo kwa Everton ambapo wameshinda mechi mbili tu za ligi msimu huu wakishika pia mkia kwenye kundi E katika michuano ya Europa ikikubali vipigo viwili kwenye mechi tatu na kutoka sare moja.

Koeman anakuwa kocha wa pili kutimuliwa ndani ya mwezi mmoja baada ya Craig Shakespeare wa Leicester City kutimuliwa mapema mwezi huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top