SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: GIGGS ATAMANI KIBARUA CHA KOEMAN EVERTON
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyota wazamani wa Manchester United Ryan Giggs amethibitisha kuwa anatamani kupewa kibarua cha kuzinoa timu za Everton na  Leicester City ...
Nyota wazamani wa Manchester United Ryan Giggs amethibitisha kuwa anatamani kupewa kibarua cha kuzinoa timu za Everton na  Leicester City baada ya kutimua makocha wao.

Everton wamemtimua Ronald Koeman mchana wa leo baada ya kipigo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal na kuwa miongoni mwa timu mbili zilizo chini ya msimamo.

Kwa upande wa Leicester walimtupia virago kocha wao Craig Shakespeare siku sita zilizopita baada ya kuboronga na sasa wanashika nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi huyo.

Giggs, ambaye ni mmiliki mwenza wa klabu ya Salford City alifungua milango wazi ya kutaka kufundisha timu kubwa tangu alipo ondoka  United alipokuwa kocha msaidizi wa Luis van Gaal lakini kuwasili kwa Jose Mourinho kulimfanya raia huyo wa Wales kutimka.

 "Ukiziangalia timu zote mbili, Leicester walikuwa mabingwa wa ligi misimu miwili iliyopita, Everton ni timu yenye historia kubwa, kwa upande wangu hizi ni klabu ambazo ningependa kuzifundisha.

"Pamoja na uwepo wa makocha wengi ambao hawana kazi lakini nina tamani kupata moja ya nafasi hizo," alisema Giggs.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Na yeye akikutana na Bab Wenger kipigo kipo palepale.....na yeye atatimuliwa hahaaaaaa

    ReplyDelete

 
Top