SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NI RONALDO TENA! 'ZIZZOU',BUFFON,GIROUD NAO WANG'ARA TUZO ZA DUNIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Cristiano Ronaldo amechaguliwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo akiwapiku mpinzani wake Lionel Messi na Neymar katika hal...
Cristiano Ronaldo amechaguliwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo akiwapiku mpinzani wake Lionel Messi na Neymar katika halfa iliyofanyika katika jiji la London nchini Uingereza.

Msimu uliopita Ronaldo aliiwezesha timu yake ya Real Madrid kuchukua taji la La Liga na ligi ya mabingwa barani Ulaya huku akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 12.
Kocha wake Zinedine Zidane 'Zizzou' amechaguliwa kocha bora akiwashinda Antonio Conte wa Chelsea na Massimiliano Allegri wa Juventus.

Mlinda mlango mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon ametwaa tuzo ya kipa bora akiwapiku Manuel Nuer wa Bayern Munich na Kaylor Navas wa Real.

Mshambuliaji Oliver Giroud ndiye mchezaji pekee kutoka katika ligi ya Uingereza ya Uingereza kupata tuzo baada ya kushinda goli bora la mwaka. Mashabiki wa Celtic walipata tuzo ya mashabiki bora wakiwapiku wale wa Borussia Dortmund.
Madrid wametoa wachezaji watano kwenye kikosi bora cha Ulaya ambao ni Marcelo, Sergio Ramos, Toni Kroos, Luca Modric na Ronaldo.

Kikosi kamili kilichotangazwa Buffon, Dani Alves, Marcelo, Ramos, Leonard Bonucci,Modric,Kroos,Andres Iniesta,Messi,Neymar na Ronaldo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top