SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: 24 WAITWA STARS KUJIWINDA DHIDI YA BENIN
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakacho jiandaa na mchezo wa kirafiki ...
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakacho jiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi Benin utakaofanyika nchini humo Novemba 11.

Mchezo huo upo kwenye kalenda ya FIFA ambapo kama Stars itashinda itapanda kwenye viwango vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho hilo.

Kikosi kilichotangazwa na kocha huyo wa zamani wa timu za Tanzania Prisons na Mtibwa makipa ni Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhan Kabwili.

Walinzi ni Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Boniface Maganga, Abdi Banda, Kelvin Yondani na Nurdin Chona.

Viungo ni Himid Mao,Hamis Abdallah, Raphael Daud, Mohammed Issa, Mzamiru Yassin, Simon Msuva, Farid Mussa na Ibrahim Ajib. Washambuliaji ni Mbwana Samata, Mbaraka Yusuph na Elius Maguri.

Kocha Mayanga amewajumuisha pia kikosini wachezaji watatu vijana ambao ni Yohana Mkomola, Abdul Mohammed na Dickson Job.

Stars itaingia kambini Novemba 5 kujiandaa na mchezo huo na watasafiri kuelekea Benin Novemba 9.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Mbona kikosi kimetangazea mapema sana inakuwa kama usajili kwamba isije wakasajiliwa na timu nyingine.....unaita mchezaji kabla hata game zao za ligi na team zao hawajacheza?
    Wakipata injury daaah haya bhana Mayanja

    ReplyDelete
  2. Tatizo si kikosi ila binafsi naamini ni uwezo mdogo wa kocha ktk kuunganisha wachezaji na kujenga timu ya sasa na hata baadae pia

    ReplyDelete
  3. Hatuna kocha hapo ni maigizo

    ReplyDelete
  4. Kuitwa mapema kwa kikosi sio ishu ,na ni jambo la kawaida hata wenzetu wanafanya hivyo

    ReplyDelete

 
Top