Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mwisho wa kununua tiketi za mechi hiyo ni Ijumaa.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mashabiki wenye nia ya kushuhudia mechi hiyo wawahi kununua tiketi mapema kabla ya siku hiyo kwakua siku ya mchezo hakutakuwa na zoezi hilo.
"Ijumaa ndio mwisho wa kuuza tiketi kwahiyo kama kuna mtu anataka kushuhudia mchezo huo moja kwa moja anapaswa kununua siku moja kabla. Siku ya Jumamosi hakutakuwa na muda wa kuuza tiketi," alisema Lucas.
Lucas amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa kinacho subiriwa ni muda kufika.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru ambapo viingilio ni sh 20,000 kwa jukwaa kuu na 10,000 kwa mzunguko.
MWISHO WA KUNUNUA TIKETI ZA SIMBA,YANGA IJUMAA
Title: MWISHO WA KUNUNUA TIKETI ZA SIMBA,YANGA IJUMAA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Shirik...
Wasimame kwenye maneno yao maana kuongea rahisi........uwanja wa Okwi huu mtani jiandae
ReplyDeleteWAONGO HAO BHANA!
ReplyDeleteWAKIONA HAZIJAISHA TIKETI ZAO 60000 WATAACHA KUUZA MPAKA J MOSI KWELI?
WAONGO HAO BHANA!
ReplyDeleteWAKIONA HAZIJAISHA TIKETI ZAO 60000 WATAACHA KUUZA MPAKA J MOSI KWELI?
Tiketi elfu 60 za wapi Mzee,shamba la bibi tiketi elfu 23 tu
Delete