Mkongwe Fransesco Totti amesema Cristiano Ronaldo anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanaume zitakazotolewa usiku wa leo jijini London, Uingereza.
Raia huyo wa Ureno ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka jana ameisaidia Real Madrid kutwaa taji la ligi, na ligi ya mabingwa barani Ulaya huku akiwa kinara ya ufungaji kwa kufunga mabao 12.
Ronaldo anagombania tuzo hiyo sambamba na mpinzani wake mkubwa Lionel Messi pamoja na Neymar ambaye kwa sasa anachezea Paris Saint-Germain.
"Mwisho wa siku Ronaldo ndio anastahili kutwaa tuzo mbele ya wenzake, alikuwa na msimu mzuri na ndiye mfungaji bora wa michuano ya Ulaya,"Nyota huyo wa zamani AS Roma aliuambia mtandao wa FIFA kuelekea tuzo hizo.
Kwa upande wake kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde amesema Messi ndio anayepaswa kutwaa taji hilo mbele ya Ronaldo na Neymar.
Messi, 30, amefunga jumla ya mabao 54 msimu uliopita akiisaidia Barcelona kutwaa taji la kombe la mfalme 'Copa del Rey'.
"Sote tunajua Messi ndiye mchezaji bora wa dunia kwa sasa, anastahili kupata tuzo hii," alisema Valverde.
TOTTI AMPA RONALDO BALLON D'OR
Title: TOTTI AMPA RONALDO BALLON D'OR
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mkongwe Fransesco Totti amesema Cristiano Ronaldo anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanaume zitakazotolewa us...
Hili halina ubishi kabisa
ReplyDeleteHili halina ubishi kabisa
ReplyDelete