SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KUWAONA OKWI,AJIB OKTOBA 28 BUKU KUMI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiingilio cha chini kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jumamosi ijayo kitakuwa sh 10,000....
Kiingilio cha chini kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jumamosi ijayo kitakuwa sh 10,000.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki wa soka nchini utapigwa kwenye uwanja huo badala ya ule wa taifa kutokana na kuendelea kwa ukarabati.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amevitaja viingilio hivyo kuwa jukwaa kuu itakuwa sh 20,000 na mzunguko ni sh 10,000.

"Tutakuwa na viingilio vya aina mbili pekee kwenye mchezo wa namba 58 Yanga dhidi ya Simba vitakuwa sh 20,000 kwa jukwaa kuu na sh 10,000 kwa mzunguko," alisema Lucas.

Uwanja wa Uhuru una uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000 huenda kiingilio hicho kinatokana na udogo wa dimba hilo ili kupunguza idadi ya watu siku hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top