SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MTANANGE WA SIMBA, YANGA NI 'SHAMBA LA BIBI SIO TAIFA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekanusha kuwa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utafanyika Uwanja Taifa badala yake u...
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekanusha kuwa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utafanyika Uwanja Taifa badala yake utapigwa kwenye dimba la Uhuru 'Shamba la bibi kama ilivyotoa taarifa awali.

Kumekuwa taarifa zilizokuwa zikigazaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Taifa Oktoba 28 lakini Shirikisho hilo limekanusha na kusema mchezo utapigwa Shamba la bibi.

Ofisa habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas amesema uwanja wa Taifa bado upo kwenye matengenezo hivyo mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru kama ilivyo tangazwa awali.

"Mchezo namba 58 kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Simba utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru na sio Taifa kama ilivyoripotiwa na mitandao mbalimbali ya kijamii," alisema Lucas.

Mapema mwezi huu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Serikali haitaruhusu kutumika kwa Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 mpaka ukarabati wake ukamilike kabisa.

Lucas ametaja viingilio kwenye mchezo huo kuwa jukwaa kuu itakuwa sh 20,000 na mzunguko ni sh 10,000.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top