Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza kwenye ligi msimu huu baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Kagera wameondoka mkiani mwa msimamo baada ya kufikisha pointi sita na kumpa ahueni kocha Meck Mexime baada ya kutafuta ushindi kwa muda mrefu.
Kagera ambayo ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya tatu haikuwa vizuri katika michezo saba ya awali ya ligi iliyoanza mwezi Agosti lakini ushindi wa leo utarudisha ari kwa wachezaji na kuendelea kupambana kujiweka katika nafasi nzuri.
Wakati huo huo Mtibwa Sugar imeshindwa kuishusha Simba kileleni mwa msimamo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Singida United mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu.
Mtibwa imefikisha pointi 16 sawa na timu za Simba, Yanga na Azam lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanabaki kileleni kutokana na uwiano wa mabao ya kufungwa.
Lipuli nayo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Samora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa.
Matokeo ya mechi la ligi zilizopigwa leo
Kagera Sugar 2-1 Ndanda FC
Lipuli FC 2-1 Mbao FC
Mtibwa Sugar 0-0 Singida United
Njombe Mji 0-0 Stand United
Majimaji 1-1 Mwadui FC
WAMEAMKA' KAGERA YAPATA USHINDI WA KWANZA VPL
Title: WAMEAMKA' KAGERA YAPATA USHINDI WA KWANZA VPL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kagera Sugar imepata ushindi wa kwanza kwenye ligi msimu huu baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja...
HAO ILITAKIWA WAPIGWE MECHI ZOTE MPAKA LIGI INAISHA.
ReplyDeleteHAO ILITAKIWA WAPIGWE MECHI ZOTE MPAKA LIGI INAISHA.
ReplyDelete