SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: POGBA AZIDI KUMPASUA KICHWA MOURINHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatarajia kurejea uwanjani kwa beki wake Marcos Rojo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa m...
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatarajia kurejea uwanjani kwa beki wake Marcos Rojo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi Novemba lakini hajui kiungo  Paul Pogba atapona lini.

Kiungo huyo raia wa Ufaransa amekuwa nje ya uwanja tangu  Septemba 12 alipapata maumivu ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya FC Basel, wakati Rojo aliumia mwezi  Aprili na hakucheza mechi yoyote msimu huu.

Mourinho amesema ana uhakika wa Rojo kurejea siku chache zijazo kwa sababu anafanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha kwanza, lakini Pogba hajui kwakua bado anafanya mazoezi peke yake.

"Marcos anafanya mazoezi na Mimi, na kwa sababu hiyo naweza kusema atarejea uwanjani baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

"Sijui Pogba atarejea lini uwanjani, hafanyi mazoezi na mimi anafanya mwenyewe. Kama mchezaji hayupo kwenye kundi langu inakuwa ngumu kujua lini hasa anaweza kuwa fiti," alisema raia huyo wa Ureno.

United itaikaribisha Benifica katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford kesho.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top