SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MTIBWA KUISHUSHA SIMBA LEO?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Mtibwa Sugar ina nafasi ya kuongoza ligi kuu ya Vodacom endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wake dhidi ya Singida United utak...
Timu ya Mtibwa Sugar ina nafasi ya kuongoza ligi kuu ya Vodacom endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wake dhidi ya Singida United utakaofanyika kwenye uwanja wa Manungu Complex jioni ya leo.

Mtibwa yenye pointi 15 ikishinda itakuwa na alama 18 na kuizidi Simba pointi mbili ambayo ipo sawa na Yanga na Azam ikiwa na uwiano wa mabao ya kufunga.

Msemaji wa 'Wakata Miwa' hao Thobias Kifaru amenukuliwa akisema  katika mchezo wao wa leo watapigana kufa na kupona kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kupaa kwenye msimamo wa ligi.

"Singida ni timu nzuri na imefanya usajili mkubwa msimu huu lakini tumejipanga kuibuka na ushindi ili kuwa vinara kwenye msimamo baada ya Simba kutoka sare na Yanga," alisema Kifaru.

Mchezo mwingine Kagera Sugar itakuwa uwanja wa Kaitaba kuikaribisha Ndanda FC katika mchezo ambao wanapaswa kupata ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huu.

Kagera ina pointi tatu ikiwa inaburuza mkia ikitoka sare michezo mitatu pekee bila kuonja radha ya ushindi mpaka sasa.

Ratiba ya mechi za ligi kuu leo

Lipuli FC vs Mbao FC
Kagera Sugar vs Ndanda FC
Majimaji vs Mwadui FC
Mtibwa Sugar vs Singida United
Njombe Mji vs Stand United

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top