SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KICHUYA AFUNGUKA KUHUSU KUWAFUNGA YANGA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Winga wa timu ya Simba, Shiza Kichuya amesema inatokea tu kuwafunga Yanga wala hajipangi ni Mungu mwenyewe humuwezesha kufanya hivyo. Mc...
Winga wa timu ya Simba, Shiza Kichuya amesema inatokea tu kuwafunga Yanga wala hajipangi ni Mungu mwenyewe humuwezesha kufanya hivyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amefunga katika mechi tatu mfululizo dhidi ya Yanga tangu ajiunge na Wekundu hao msimu uliopita.

Katika mchezo wa jana Kichuya alifunga bao la uongozi kwa Simba akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Erasto Nyoni dakika ya 57 ambalo lilidumu kwa dakika tatu pekee kabla ya Yanga kusawazisha.

"Huwa inatokea kuwafunga Yanga, ninapata nafasi na ninafunga namshukuru Mungu kwa hilo," alisema Kichuya.

Oktoba mosi mwaka Kichuya alifunga bao la kusawazisha la mpira wa kona lililoingia moja kwa moja wavuni dakika za majeruhi na kufanya mchezo huo uliokuwa na vurugu kumalizika kwa sare ya bao moja.

Kichuya ameifikia rekodi ya Amiss Tambwe wa Yanga ambaye nae alifunga dhidi ya Simba mechi tatu mfulizo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top