SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: CHELSEA YAKAMILISHA USHINDI WA VIGOGO UINGEREZA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya AFC Bournemouth na kuzifanya klabu zote kubwa nchini Uingereza kupata matokeo ya ...
Timu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya AFC Bournemouth na kuzifanya klabu zote kubwa nchini Uingereza kupata matokeo ya ushindi wikiendi hii.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Vitality bao hilo pekee la Chelsea lilifungwa na nyota Eden Hazard dakika ya 51.

Mchezo wa mapema Manchester United iliibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford huku bao hilo likifungwa na Anthony Martial.
Arsenal nao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swansea City wakati Man City ikiichapa West Bromwich Albion mabao 3-2.

Liverpool ambayo wiki iliyopita ilikubali kichapo kikubwa kutoka kwa Spurs leo imeibugiza Huddersfield Town mabao 3-0 katika uwanja Anfield.
Matokeo kamili ya mechi za EPL leo

Man United 1-0 Tottenham Hotspur

Arsenal 2-1 Swansea City

Crystal Palace 2-2 West Ham United

Liverpool 3-0 Huddersfield Town

Watford 0-1 Stoke City

West Bromwich 2-3 Man City

AFC Bournemouth 01 Chelsea

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top