Winga Shiza Kichuya amepewa zawadi ya shilingi laki tatu na mashabiki wa timu ya Simba kutoka tawi la Simba kwanza baada ya kuibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Yanga mchezo uliyofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Kichuya alifunga bao la Simba kwenye mchezo huo dakika ya 57 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Yanga.
Tangu ajiunge na Wekundu hao msimu uliopita Kichuya amefunga mechi zote tatu alizocheza dhidi ya Yanga hali inayokonekana kuwa bado mabingwa hao hawajapata njia ya kumzuia.
Mratibu wa Simba Kwanza Tarik Hashim amesema kila mchezo wa Simba watatoa kiasi cha fedha kwa ajili ya mchezaji bora na Kuchuya amekuwa wa tatu kupata tuzo hiyo.
"Tumemkabidhi Kichuya shilingi la tatu baada ya kuwa mchezaji bora wa mechi na tutaendelea kutoa zawadi katika kila mechi," alisema Tarik.
Wachezaji waliwahi kuchukua kitita kutoka Simba Kwanza ni John Bocco 'Adebayor' na Erasto Nyoni.
KICHUYA ALAMBA NOTI ZA SIMBA KWANZA
Title: KICHUYA ALAMBA NOTI ZA SIMBA KWANZA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Winga Shiza Kichuya amepewa zawadi ya shilingi laki tatu na mashabiki wa timu ya Simba kutoka tawi la Simba kwanza baada ya kuibuka mcheza...
Post a Comment