SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: UHONDO WA LIGI YA MABINGWA KUENDELEA KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kivumbi cha ligi ya mabingwa barani Ulaya kitaendelea tena kwa michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali. Manchester United itak...
Kivumbi cha ligi ya mabingwa barani Ulaya kitaendelea tena kwa michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Manchester United itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford kuikaribisha Benifica ya Ureno katika mchezo wa kundi A. United ndio kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu.

Chelsea itakuwa ugenini kucheza na AS Roma ya Italia ambapo katika mchezo wa mwisho timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3 katika uwanja wa Stamford bridge.

Paris Saint Germain ya Ufaransa itakuwa nyumbani Parc des Princes kuikakaribisha Anderlecht ya Ubelgiji katika mchezo wa kundi B. Mchezo mwingine wa kundi hilo Celtic itaikaribisha Bayern Munich.

Barcelona nao watakuwa ugenini kucheza na Olympiacos ya Ugiriki huku Sporting CP ya Ureno ikicheza na Juventus ya Italia.

Ratiba kamili ya mechi za kesho za ligi ya mabingwa

Basel vs CSKA Moscow

Manchester United vs  Benfica

Celtic vs Bayern Munich

Paris Saint Germain vs Anderlecht

Atletico Madrid vs Qarabag FK

Roma vs Chelsea

Olympiacos vs Barcelona

Sporting CP vs Juventus

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. CHELSEA WAJIANGALIE HAPO WAKIFANYA UTANI WANAPIGWA.

    ReplyDelete
  2. CHELSEA WAJIANGALIE HAPO WAKIFANYA UTANI WANAPIGWA.

    ReplyDelete

 
Top