SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SPURS,ARSENAL ZATOA VIPIGO VIKUBWA EPL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kibarua cha kocha Jurgen Kloop ndani ya Liverpool kipo hatiani kutokana na mwenendo ambao sio mzuri baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-1 ...
Kibarua cha kocha Jurgen Kloop ndani ya Liverpool kipo hatiani kutokana na mwenendo ambao sio mzuri baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Tottenham Hotspur.

Safu ya ulinzi ya Majogoo hao wa Anfield imekuwa ikiruhusu mabao mengi kitu ambacho mabosi wa Liverpool wanaweza wakashindwa kumvumilia kocha huo.

Wiki iliyopita vijana hao wa Kloop walilazimishwa sare ya bila kufungana na Manchester United huku wakitawala kila idara ila wakashindwa kupata bao.

Mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley ulishuhudia wenyeji wakitawala sehemu kubwa huku mshambuliaji Harry Kane akifunga mabao mawili wakati mengine yalifungwa na Dele Alli na Son.
Arsenal nayo imeibugiza Everton mabao 5-2 huku ikionyesha kiwango safi mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Godson Park.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Nancho Monreal, Alexander Lacazzate, Mesut Ozil, Aaron Ramsey na Alex Sanchez na huo ndio mchezo wa kwanza wa 'Washika bunduki' hao kushinda ugenini.

Ushindi huo nao umeendelea kukiweka rehani kibarua cha kocha Ronald Koeman ambaye hana mwenendo mzuri kutokana na vipigo mfufulizo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top