Timua timua ya makocha imeendelea kuchukua nafasi kubwa barani Ulaya baada ya hii leo klabu ya Rangers ya Scotland kumtupia virago kocha wake Pedro Caixinha aliyedumu kwa miezi saba pekee.
Kocha Graeme Murty atakaimu nafasi hiyo kama alivyofanya kabla Caixinha hajapewa kibarua hicho mwezi Machi mwaka huu.
Caixinha, 46, ameshinda mechi 14 katika michezo 26 ambapo kocha msaidizi Helder Baptista na makocha wengine Pedro Malta na Jose Belman wote wametimka klabuni hapo.
Maamuzi hayo yamefanywa na kikao cha dharula cha bodi ya klabu hiyo kilichofanyika leo kufuatia sare ya bao moja waliyopata dhidi ya Kilmarnock nakuifanya Rangers kushuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi. Jumapili iliyopita Rangers ilipoteza mchezo wa nusu fainali wa kombe la ligi.
"Tutatangaza kocha mpya haraka iwezekavyo lakini bodi inatafuta kocha bora ambaye ataweza kuingoza Rangers na kuilinda brand ya timu na mashabiki wake," Ilisomeka taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.
Rangers ipo alama nane nyuma dhidi ya vinara Celtic baada ya mechi 10.
RANGERS NAYO YAMTIMUA KOCHA WAO
Title: RANGERS NAYO YAMTIMUA KOCHA WAO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timua timua ya makocha imeendelea kuchukua nafasi kubwa barani Ulaya baada ya hii leo klabu ya Rangers ya Scotland kumtupia virago kocha w...
NA TAREHE 28 JUMAMOSI ITAKUWA ZAMU YA TIMU KUBWA TANZANIA KUMTIMUA KOCHA.
ReplyDelete