SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: HUU HAPA MTIHANI WA OKWI,AJIB 'DERBY' YA KARIAKOO KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Saa chache zimebaki kabla ya kufanyika mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi mechi ya watani wa jadi ...
Saa chache zimebaki kabla ya kufanyika mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga. Katika mchezo huo utakaofanyika kwenye uwanja wa Uhuru saa 10 jioni Yanga ndio timu mwenyeji.

Timu hizo zina pointi 15 kila moja lakini Simba wapo kileleni kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga. Kivutio kikubwa kwenye mchezo wa kesho kitakuwa uwepo wa washambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Ibrahim Ajib kwa Yanga.

Okwi ndiye kinara wa ufungaji mpaka sasa akiwa amefunga mabao nane huku Ajib akifunga matano na ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika timu yake ya Yanga.

Pamoja na uwezo mkubwa wa ufungaji walio uonyesha nyota hao tangu kuanza msimu huu, lakini wana mtihani mkubwa wa kuvunja rekodi iliyowekwa na Abdallah Kibadeni ya kufunga 'hat trick' katika mechi ya watani wa jadi.
Kibadeni alifunga hat trick hiyo Julai 19,1977 wakati Simba ikishinda mabao 6-0, rekodi ambayo haijawi kuvunjwa na mchezaji yoyote mpaka sasa kitu ambacho ni mtihani kwa Okwi na Ajib ambao wanaaminiwa sana timu zao kutokana na umahiri waliuonyesha msimu huu.

Okwi alikaribia kuivunja rekodi hiyo Mei 6, 2012 alipofunga mabao mawili huku akishiriki kikamilifu katika upatikanaji wa mengine matatu wakati Simba ikiifunga Yanga mabao 5-0. Okwi amekuwa hatari zaidi msimu huu hasa anapokuwa katika uwanja wa Uhuru kitu ambacho walinzi wa Yanga wanapaswa kuwa makini nae.

Ajib ambaye msimu uliopita alikuwa Simba ameonyesha utofauti mkubwa wa kiuchezaji akiwa na mabingwa hao wa kihistoria huku akifunga mabao mawili ya kufanana kwa mtindo wa mpira wa adhabu upande wa kushoto kitu ambacho Wekundu hao wanapaswa kuwa makini sana.

Rekodi ya Kibadeni ina miaka 40 sasa ambapo wachezaji nyota wengi wamepita katika timu hizo kwa nyakati tofauti lakini wameshindwa kuivuja rekodi hiyo.
Wachezaji ambao walifunga mabao mawili katika mechi ya watani wa jadi katika michezo ya ligi kuu tangu Kibadeni aweke rekodi hiyo ni Jumanne Hassan 'Masimenti',Dua Said, Stephen Mapunda 'Garincha', Emmanuel Gabriel, Nico Nyagawa, Mussa Mgosi na Okwi kwa upande wa Simba.

Kwa Yanga waliofunga mabao mawili kwenye 'derby' hiyo ni Said Mwamba Kizota, Idd Moshi 'Mnyamwezi', Jerryson Tegete na Hamis Kiiza 'Diego'.

Mtihani huu sio wa Okwi na Ajib pekee unawahusu pia wakina Amiss Tambwe, Donald Ngoma, Laudit Mavugo na John Bocco. Swali ni je kuna atakaye weza kuvunja rekodi hii kesho? Tusubiri na kuona.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top